sw_obs/content/40.md

2.4 KiB

40. Yesu Anasulubiwa

OBS Image

Baada ya askari kumdhihaki Yesu, walimpeleka kumsulibisha. walimlazimisha aubebe msalaba ambao ungetumika kumuua.

OBS Image

Askari walimpeleka Yesu eneo liitwalo "fuvu la kichwa" wakaipigilia miguu na mikono yake msalabani. Lakini Yesu akasema, "Baba wasamehe, kwa sababu hawajui wanalotenda." Pilato akaagiza waandike kwamba, "Mfalme wa Wayahudi" ikiwa ni ishara; na waweke msalabani, juu ya kichwa cha Yesu.

OBS Image

Askari walipigia kura mavazi yake. Na kitendo hiki kinatimiza unabii usemao kwamba, " wakagawana nguo zangu na kucheza kamali."

OBS Image

Yesu alisulibiwa katikati ya wanyang'anyi wawili; mmojawapo alimdhihaki Yesu, lakini mwingine alisema, "Humwogopi Mungu!? Sisi tunahatia, lakini huyu hana hatia" Ndipo yeye akamwabia Yesu "Tafadhali unikumbuke katika ufalme wako" Yesu akamjibu, leo, utakuwa nami Paradiso."

OBS Image

Viongozi wa wayahudi na baadhi ya wengine katika umati walimdhihaki Yesu. Wakisema, "kama wewe ni Mwana wa Mungu, shuka msalabani, jiokoe mwenyewe, ndipo tutakuamini."

OBS Image

Ndipo katika eneo hilo kukawa giza nene, ingawa ilikuwa mchana. Mchana huo kukawa giza kwa saa tatu.

OBS Image

Yesu akalia, "Baba imekwisha naweka mikononi mwako roho yangu." Ndipo akainama akajitoa mwenyewe roho yake. Alipokufa lilitokea tetemeko la ardhi na pazia la hekaluni lililowatenga watu na Mungu lilipasuka vipande viwili, tokea juu hadi chini.

OBS Image

Kifo chake Yesu kinafungua njia ili watu waje kwa Mungu. Askari aliyemlinda Yesu alipoona mambo haya yote yanatokea alisema, "Hakika mtu huyu hakuwa na hatia, alikuwa Mwana wa Mungu."

OBS Image

Na ndipo Yusufu na Nikodemo viongozi wa Wayahudi walioamini Yesu kuwa ni Masihi wakauomba mwili wa Yesu na kuufunga kwenye sanda na kupeleka kwenye kaburi lililochongwa tayari mwambani na wakasogeza jiwe kubwa kulifunga kaburi.

Simulizi ya Biblia kutoka: Mathayo 27:27-61; Marko 15:16-47; Luka 23:26-56; Yohana 19: 17-42