sw_obs/content/37.md

3.0 KiB

37. Yesu Amfufua Lazaro kutoka Wafu

OBS Image

Siku moja, Yesu alipata habari kuwa Lazaro ni mgonjwa sana. Lazaro na dada zake wawili- Martha na Maria walikuwa marafiki wa karibu wa Yesu. Yesu alipopata habari hizi alisema, "Huu si ugonjwa wa kifo, bali ni ugonjwa wa kumtukuza Mungu." Yesu aliwapenda marafiki zake, lakini alisubiri hadi siku mbili.

OBS Image

Baada ya siku mbili, Yesu aliwaambia wanafunzi wake, ''Twendeni tena Uyahudi." "Lakini mwalimu. " Wanafunzi wake walisema, "Muda mfupi tu uliopita watu walitaka kukuua!" Yesu alisema "Rafiki yetu Lazaro amelala usingizi na ni lazima nimwamshe."

OBS Image

Wanafunzi wa Yesu walijibu, "Bwana, kama Lazaro amelala, basi atapata nafuu." Yesu aliwaambia wazi, "Lazaro amekufa, nafurahi kuwa sikuwepo ili mpate kuniamini."

OBS Image

Yesu alipofika katika mji wa Lazaro, Lazaro alikuwa tayari amekufa kwa siku nne. Martha alikwenda kumwona Yesu akasema, "Bwana, kama ungekuwa hapa, kaka yangu asingekufa . Lakini ninaamini kuwa Mungu atakupa chochote umwombacho."

OBS Image

Yesu akajibu akasema, "Mimi ni Ufufuo na Uzima, yeyote aniaminiye ataishi, hata kama akifa. Kila aniaminiye hatakufa. Unaamini hivyo?" Martha akajibu, "Ndiyo Bwana ninaamini kuwa wewe ni Masihi, Mwanawa Mungu."

OBS Image

Maria alipofika. Alianguka miguuni pa Yesu akasema, "Bwana, kama wewe tu ungekuwepo kaka yangu asingekufa." Yesu akawauliza, "Mmemuweka wapi Lazaro?" Walimjibu " Kaburini, njoo uone." Yesu alilia.

OBS Image

Kaburi lilikuwa pango limefunikwa na jiwe. Yesu alipofika kaburini aliwaambia, "Liondoeni jiwe." Lakini Martha alisema, "Amekuwa kaburini sasa siku nne, ananuka!"

OBS Image

Yesu alijibu, "Je, sikusema kuwa kama ukiniamini utaona utukufu wa Mungu?" Ndipo wakaliondoa jiwe.

OBS Image

Basi Yesu alitazama juu mbinguni akasema, "Baba, asante kwa kuwa unanisikia. Tena najua wewe hunisikia siku zote. Lakini nimesema haya kwa ajili ya watu hawa waliosimama hapa, kwa kuwa wataamini kuwa ulinituma." Kisha Yesu akapaza sauti, "Lazaro, njoo nje."

OBS Image

Ndipo Lazaro alitoka nje! Alikuwa bado amefungwa sanda, Yesu akawaambia, "Msaidieni kuondoa sanda na mwacheni huru!." Wayahudi wengi walimwamini Yesu kwa sababu ya muujiza huu.

OBS Image

Lakini viongozi wa dini ya kiyahudi waliona wivu, ndipo wakakusanyika pamoja kupanga watakavyoweza kumuua Yesu na Lazaro.

Simulizi ya Biblia kutoka: Yohana 11:1-46