sw_obs/content/28.md

2.5 KiB

28. Kijana Tajiri Kiongozi

OBS Image

Siku moja, kiongozi kijana tajiri alimwendea Yesu na kumuuliza, "mwalimu mwema nifanye kitu gani cha lazima ili niwe na uzima wa milele?" Yesu akamwambia, "kwanini unaniita mwema?" Kuna mmoja tu aliye mwema naye ni Mungu. Lakini ukitaka kuwa na uzima wa milele, tii sheria za Mungu.

OBS Image

"Ni mambo gani nahitaji kutii?" Aliuliza. Yesu akajibu, "usiuwe. Usizini. Usiibe. Usidanganye. Mheshimu baba yako na mama yako, na umpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.

OBS Image

Lakini kijana akasema, "Nimezitii sheria hizo zote tangu nikiwa kijana. Je, nahitaji kufanya nini bado ili niishi milele? Yesu alimwangalia na akampenda.

OBS Image

Yesu akajibu, kama unataka kuwa mkamilifu, nenda ukauze kila kitu ulichonacho na utoe pesa kwa maskini, na utakuwa na hazina mbinguni, kisha njoo unifuate.

OBS Image

Yule kijana aliposikia alichokisema Yesu, alihuzunika sana, kwa sababu alikuwa tajiri sana na hakutaka kutoa vitu vyote alivyomiliki. Akageuka na akaenda mbali na Yesu.

OBS Image

Kisha Yesu akawaambia wanafunzi wake, "Ni vigumu sana kwa watu matajiri kuingia katika ufalme wa Mungu! Ndiyo, ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano kuliko mtu tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu

OBS Image

Wanafunzi waliposikia alichosema Yesu, walishikwa na mshangao na kusema, "Ni nani basi anaweza kuokolewa?"

OBS Image

Yesu akawatazama wanafunzi na kusema, "Kwa watu mambo haya hayawezekani, lakini kwa Mungu mambo yote yanawezekana".

OBS Image

Petro akamwambia Yesu, "Tumeacha kila kitu na kukufuata wewe. Je, tutapata thawabu gani?"

OBS Image

Yesu akajibu, "Kila mmoja aliyeacha nyumba, kaka, dada yake, baba, mama, watoto, au mali kwa ajili yangu atapokea mara 100 zaidi na pia atapokea uzima wa milele. Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho, na wengi walio wa mwisho watakuwa wa kwanza."

Simulizi ya Biblia kutoka: Mathayo 19:16-30; Marko 10:17-31; Luka 18:18-30